Mark 11:12-14

12 aKesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, Isa alikuwa na njaa. 13Akauona mtini kwa mbali, naye akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini. 14 bAkauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.

Isa Atakasa Hekalu

(Mathayo 21:12-17; Luka 19:45-48; Yohana 2:13-22)

Copyright information for SwhKC